LIGI DARAJA LA PILI (SDL) KUANZA OKTOBA 17
Kwa
kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya Ligi Daraja la Pili (SDL)
yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) hivi karibuni, SDL kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa
katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na
ugenini.
Timu itakayoongoza kundi itacheza
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2016/2017 wakati ya mwisho katika
kila kundi itarudi kucheza Ligi ya Mkoa wake kwa msimu wa 2016/2017.
Makundi ya SDL ni kama ifuatavyo;
Kundi A ni Abajalo FC (Tabora), Singida United (Singida), Mvuvuma FC
(Kigoma), Milambo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam) na Transit
Camp (Dar es Salaam).
Timu zinazounda kundi B ni
Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba FC (Mwanza), AFC
Arusha, Madini FC (Arusha) na Alliance Schools (Mwanza).
Kundi C ni Kariakoo (Lindi),
Mshikamano FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Abajalo FC
(Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers (Dar es Salaam) na Villa Squad
(Dar es Salaam).
Nazo African Wanderers (Iringa),
Mkamba Rangers (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma), Wenda FC (Mbeya),
Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya) na Sabasaba United (Morogoro) zitakuwa kundi
D.
Klabu nyingi bado hazijatuma jina
la uwanja wa nyumbani, hivyo zinakumbushwa kufanya hivyo haraka ili
kurahisisha upangaji wa ratiba.
Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016 inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
Post a Comment