KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAWAFUTURISHA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA
Baadhi ya wakina dada wakiwa wamejiweka sawa kuwapokea wageni mbalimbali ambao walifika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya kwa ajili ya Kufuturu.
Baadhi ya wadau wakiwa wanangoja muda wa kufuturu ufike.
Bw. Francis Mwasamwene Meneja wa Mauzo Tigo Mkoa wa Mbeya ambaye pia alikuwa mratibu wa kufanikisha Shughuli hii ya Kuwafuturisha wakazi wa Mbeya akiongea Machache.
Meneja wa Tigo Pesa Kanda ya Njanda za Juu Kusini Thomas Meitaron akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Tigo kwa wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali Dini kwa kujitokeza na kufuturu pamoja, alisema Tigo ni Sehemu ya Familia ya wanambeya na pia Waislam kwa ujumla ndio mana wafanyakazi na wananchi wa Mbeya wamejumuika Pamoja kufuturu, Mwisho alisisitiza kuwa sasa huduma za Tigo zimeboreshwa na zimemfikia kila mmoja.
Sheigh Ally Hassan Furukutu ambaye ni Katibu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya , akiwashukuru Tigo kwa Moyo waliojitolea kuwafuurisha wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali Dini wala Kipao cha mtu, na aliahidi ushirikiano mzuri kati ya Tigo na Waislam, Mwisho alitoa Dua kwa wote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi (wa kwanza kushoto) akipata futari pamoja na wegeni wengine walioalikwa kufuturu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo pamoja na wakazi mbalimbali kutoka jijini Mbeya wakichukua Futari ambayo iliandaliwa na kampuni la Tigo Tanzania.
Baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo watumishi waserikali, wananchi na wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Tigo wakiendelea kupata Futari.
Baadhi ya wakina dada na akina mama wakiendelea kupata Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya simu ya Tigo.
Wakiendelea kupata futari.
Picha ya Pamoja baada ya Kumaliza Kufuturu.
Post a Comment