JESHI LA POLISI LAWATIA MBARONI, VIONGOZI WA CHADEMA KWA KUKUTWA NA MASHINE YA BVR
Jeshi
la polisi wilayani kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya
BVR ikitumika kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa
mwenyekiti wa mtaa wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce kupitia
CHADEMA.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amesema
tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa nyakato
ambapo mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga
kura.
Mpesya
amesema kuwa vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka
kwa raia wema ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na
vitambulisho vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika
kuandikishwa.
Ameongeza
katika harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata
mhamiaji haramu mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa
ameshaandikishwa na mashine hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti
huyo wa mtaa.
Mpesya
amesema jeshi la Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa
mtendaji wa kata ya Nyasubi Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana
ya kusimamia mashine hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika
nyumbani kwa myekiti wa mtaa.
Katika
hatua nyingine Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa
kukanusha taarifa hiyo, kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya
serikali na kwamba wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa
kukamatwa kwa mashine hiyo upo kituo cha polisi.
Tangu
kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu
la wapiga kura wilayani humo hilo ndio tukio la kwanza la aina yake
ambalo limevuta hisia, na Mpesya amesema jeshi la polisi bado
linaendelea na uchunguzi.
Post a Comment