HATIMAE BARAZA LA MADIWANI, MANISPAA YA KINONDONI LAAHIRISHWA RASMI
Rais Mstaafu wa awamu ya pili ,
Alhaji Ally Hassan Mwinyi, akimkabidhi Jezi mstahiki meya wa manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, wakati wa hafla ya kuvunja baraza la madiwani la Manispaa
ya Kinondoni.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Alli Hassan Mwinyi, akikagua maonyesho ya kazi zinazofanywa na manispaa ya Kinondoni.
Rais Mstaafu wa awamu
ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na na nishani ya
utumishi uliotukuka Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph
Mwenda wakati wa sherehe zakufunga barza la manispaa hiyo.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza
la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa
mheshimiwa Rais mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli hizo zilianza kwa kikao
cha baraza cha kawaida cha kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada
ya hapo aliwasili mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
na kufuatiwa na tukio la kupita katika mabanda maalum yaliyoandaliwa
yakionyesha shughuli za kila idara na kupata maelezo ya shughuli
zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na mafanikio mbalimbali katika
idara hizo.
Baada ya mgeni rasmi kupita katika mabanda hayo na kupata
maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha kusitisha rasmi
baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha utambulisho
uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi
mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.
Akiongea mkurugenzi wa jiji
alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali
ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni
mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania
nzima.
Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni
alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza
shughuli za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana
yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza
kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki
yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko
mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa
mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
Mgeni rasmi alitoa medani na
vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika
kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni
mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu
Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila
mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu
hiyo na kuisaidia kwa hali na mali.
Akiongea katika hafla hiyo
Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana
na suala la maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa
wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya
umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo aliiongelea pia
hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa
wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana
kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi
sasa.Akiongelea suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa
na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi
vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.
alisema Manispaa imekuwa
ikishinda mfululizo katika mashindano ya usafi yanayosimamiwa na wizara
ya afya pamoja na hilo aliongelea pia mpango kabambe wa alioucha katika
mchakato wa utunzaji wa coco beach ili kuiboresha na kubadilishwa sura
yake licha ya hayo manispaa hii pia imekuwa ikipata tuzo ya kutunza
mahesabu vizuri,Pia alimshukuru Naibu Meya Songoro Mnyonge kwa
ushirikiano na ushauri mzuri ambao amekuwa akimpa na mkurugenzi kwa
ubunifu na ushirikiano wake pamoja na watendaji wote kwa ujumla.
Kaimu
mkuu wa mkoa akiongea alipopewa nafasi alisema haihitaji hata maelezo
kuelezea Manispaa ya Kinondoni kwani juhudi zao zinaonekana kwa
macho.Mgeni rasmi akiongea katika hafla hiyo aliwashukuru kwa heshima
hiyo waliyompa kwani alikuwa ana hamu kubwa ya kuja kuonana na watendaji
wa Manispaa hii ,alisifia kazi nzuri ya kuboresha maendeleo katika
Manispaa hii na kuongeza kuwa Kinondoni ina uwezo wa kuendesha mambo
vizuri kwa kuja kwake katika hafla hii amefundishika haswa.
Hongera
Manispaa ya Kinondoni.
Post a Comment