AIRTEL SMARTFONIKA YAMFIKIA MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS FM / TV
Ofisa Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya kisasa mapema wiki hii katika duka la wazi la Airtel lililopo Game Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
Ofisa Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.
Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
Ofisa Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani City.
Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu huo.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo mkubwa.
"Tumejipanga vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.
Mmbando alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mmbando ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wa Airtel kutembelea banda lao lililopo katika viwanja hivyo ili kupata huduma mbalimbali pamoja na kujipatia simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu.
Post a Comment