Header Ads

Wizara ya Maliasili yawaonya Askari Wanyamapori Kujiepusha na Rushwa


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza  wahifadhi wa wanyamapori 103  kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kabla ya kufunga mafunzo ya jeshi Usu yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi.

.................................

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, amesema hatamvumilia mtumishi  yeyote atayejihusisha na vitendo vya rushwa kuwa ni lazima ataondolewa mara moja  ili asiendelee kuchafua taswira ya Wizara.

Alitoa rai hiyo  jana wakati akifunga mafunzo ya jeshi Usu kwa  wahifadhi wa wanyamapori  103 kutoka Mamlaka ya Hifadhi  Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori          ( TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA).

Alisema  Wizara kwa sasa  inabadili mfumo wa kiraia  na kuendesha kwa  mfumo wa kijeshi hivyo mtumishi yeyote asiyejihusisha na vitendo viovu vya namna yeyote Yule hatasalimika.

Wakati huo huo , Maj. Gen. Gaudence  Milanzi alifungua  mafunzo ya ukakamavu kwa  maafisa wanyamapori wa daraja la pili  kutoka TAWA yatakayochukua muda wa wiki tano  lengo likiwa ni kuwandaa watumishi wa taasisi hiyo katika kuboresha mbinu za kupambana na majangili.

 Akizungumza jana na wahitimu hao kabla ya kufunga  mafunzo hayo katika kituo cha Mafunzo cha Mlele mkoani Katavi ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi aliwataka  wahifadhi hao wakaoneshe kile walichojifunza kwa  kwa kujenga mahusiano mazuri na wanavijiji wanaozunguka hifadhi  nchini baadala ya kujenga uadui.

Aliwasihi wahitimu hao kutumia silaha kwa weledi pale inapobidi hasa inapohitajika kunusuru maisha ya watu na sio kuua.

Aidha,  Milanzi aliwaagiza wakuu na viongozi  wa taasisi  zote zilizo  chini ya Wizara   wahakikishe   wanashiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa Wizara inatoka kwenye mfumo wa kiraia na kuelekea kwenye  mfumo wa kijeshi katika utendaji wa shughuli za uhifadhi nchini.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, David Kanyatta aliwataka wahifadhi waliopewa mafunzo hayo wakajitume kwa kufanya kazi kwa bidii  katika vituo vyao vya kazi ili kuonesha tija kwa taifa katika uhifadhi.

Kabla ya kuwahutubia wahitimu hao, Katibu Mkuu Milanzia alioneshwa mbinu mbalimbali kwa vitendo walizojifunza katika kupambana majangili ambao wamekuwa wakitumia silaha nzito wakati wakifanya ujangili.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia)  akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103  kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Rachel Kasanda ( wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi.

Paredi ikipita mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( hayupo pichani) wakati wa  kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa  wahifadhi wa wanyamapori 103  kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. 

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa katikati) akiwa amesimama kiukakamu wakati Paredi ikipita mbele yake( haipo pichani ) kabla kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa  wahifadhi wa wanyamapori 103  kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. 

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo wakiwa wamesimama kikakamavu wakati wakila viapo vya utii na nidhamu katika utendaji wa kazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia ) akiangalia sehemu ambapo wahitimu wa mafunzo walilenga shabaha kwa kutumia risasi  ya moto kwenye picha inayoonekana wakati wa kufunga mafunzo ya wahifadhi wa wanyamapori 103  kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Rachel Kasanda ( wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi.

No comments

Powered by Blogger.