Header Ads

Mkuu wa Wilaya ya Longido DANIEL CHONGOLO ashiriki Ujenzi wa Madarasa Mawili

Mkuu wa Wilaya ya longido Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akishiriki ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani humo.
Ndugu Daniel Godfrey Chongolo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Longido akiweka Jiwe kwenye msingi wa nyumba wakati akishiriki Ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi.
....................

Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Godfrey Chongolo ameshiriki ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani Longido. 

Shule hiyo ambayo ina wanafunzi mpaka wa darasa la tano, ilikuwa na madarasa mawili tu jambo lililosababisha shughuli za utoaji elimu kwa wanafunzi kuwa ngumu. 

Katika kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa, Mkuu wa Wilaya akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw. Jumaa Mhina wamefanya kazi ya ujenzi kwa kushirikiana na wananchi siku nzima ya leo.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Wilaya ya Longido aliendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa jumla ya shilingi milioni 10.
Wananchi wilayani Longido wakiwa katika harakati za Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa kwenye shule ya Msingi Lanchi, baada ya kuhamasishwa na mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo. 
Kazi ya Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Lanchi wilayani Longido ikiendelea..
Mkuu wa Wilaya ya Longindo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akiendelea kushiriki Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Lanchi.

No comments

Powered by Blogger.