Header Ads

Msemaji wa Serikali: Waziri Hatokuwa na Mamlaka Makubwa Katika Muswada wa Habari

Serikali imesema hakutokuwa na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.

Imesema Serikali haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na  Waziri mwenye dhamana ya habari.

 Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.

Aliongeza kuwa hata katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari, Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan Ngoma.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Watangazaji wa kipindi cha Michezo cha kituo cha Redio cha CLOUDS FM cha Jijini Dar Es Salaam, kutoka kutosho Shafii Dauda (kulia) na Mbwiga mbwiguko (katikati) wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri na Waandishi wa Habari wa kituo cha habari cha Redio na Televisheni cha CLOUDS wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam,  Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.

No comments

Powered by Blogger.