Header Ads

Naibu Waziri Mhandisi HAMAD MASAUNI afanya Mazungumza na Ujumbe kutoka UNDP

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)  akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto) na Nirina Kiplagat, walipofika kwa ajili ya  kujadiliana juu  ya masuala ya amani na maendeleo.Kulia ni Katibu wa naibu waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam. 
Mshauri wa Mradi kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto), akizungumza na Naibu Waziri waWizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Watatu kushoto ni Meneja Mradi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiagana na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat (aliyeshikana naye mkono) na ) Lawrence Lachmansingh, baada ya kumaliza majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.