Header Ads

Wataalam Tanzania na Uganda wajadili Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP)

Wataalam mbalimbali kutoka Wizara  na Taasisi za Serikali za Tanzania na Uganda zinazohusika  na mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga wamekutana jijini Tanga ili kujadili masuala mbalimbali yatakayopelekea mradi huo kufanyika kwa ufanisi.

Kikao cha Wataalam hao kimehusisha pia  watendaji kutoka kampuni zitakazotekeleza  ujenzi  wa bomba hilo  ambazo ni Total E&P ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, na CNOOC ya China.

Kikao hicho cha Wataalam kitafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara zinazosimamia Sekta ya Nishati kutoka nchi Uganda  na Tanzania na baadaye Kikao cha Tatu cha Mawaziri wanaosimamia Sekta husika  kutoka nchi hizo.

Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 1443 na nchini Tanzania litapita katika mikoa ya Kagera, Geita, Tabora, Shinyanga, Dodoma, na Tanga.


Mradi huo utagharimu  Dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo bomba hilo litasafirisha mapipa 200,000 kwa siku.

No comments

Powered by Blogger.