Header Ads

Vijana Wasomi 53 Wafyatua Matofali 45,000 kwa Ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Walimu

 Vijana wasomi 53 wa grupu la Whatsapp la WAZALENDO wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 

Leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). 

Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. 

Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako.

 Mmoja wa vijana hao wasomi akielekea kazini.

  Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

No comments

Powered by Blogger.