Header Ads

Programu ya " Jiandalie Ajira " Yazinduliwa Rasmi Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akikata utepe wakati uzinduzi wa program ya JIANDALIE AJIRA inayolenga kupunguza tatizo la ajira nchini, Wengine katika picha ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese (wa pili kulia), Mwenyekiti wa bodi wa  Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani TECC Bi. Beng’I Issa (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani, Bw. Sosthenes Sambua (wa pili kushoto) na Ahmed Makbel Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira kutoka ofisi ya Waziri Mkuu (katikati).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya Jiandalie Ajira jana jijini Dar es Salaam, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa bodi wa  Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) Bi. Beng’I Issa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa (TECC) Sosthenes Sambua katikati, program hiyo ili zinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana.

Na Ally Daud-MAELEZO

Mfuko wa Kimataifa wa Vijana( Interanational Youth Foundation) imezindua rasmi programu mpya ya miaka mitano wa JIANDALIE AJIRA unaowalenga vijana hapa nchini kama moja ya jitihaha za kukuwajengea vijana mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kuondokana na tatizo la ajira .

Akizindua programu hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia ,Mhandisi Stella Manyanya alisema program hiyo ni ukombozi mkubwa kwa vijana hapa nchini kwa kuwa itawawezeshae kutengEneza ajira na kukuza uchumi.

“Programu hii  imekuja kutengneza vijana kuwa wabunifu na kutengneza ajira ikiwa ni pamoja na  kuajiri wengine na siyo kuwa wasaka ajira,”na kwa kufanya hivyo taifa litapiga hatua kiuchumi,aliongeza kusema,Mhandisi huyo ambaye  pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa” alisema Mhandisi Manyanya.

Aidha Mhandisi Manyanya aliupongeza mfuko huo wa IYF kwa kuja na mradi  ambao utatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC), Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika lisilokuwa la kiserikali la The MasterCard Foundation.

Mhandisi  Manyanya  alisema pia programu hiyo itawezesha kuwaandaa wakufunzi wa chuo cha VETA ili waweze tumika katika kuwafundisha vijana ambao ndio walengwa katika mradi mzima na ambao wanachangamoto kubwa ya ajira.

Mbali na hayo Mhandisi  Manyanya alikitaka  chuo hicho kuendeleza na kupanua wigo wa ushirikiano na waajiri ili kujenga nguvu kazi kukidhi matwakwa ya soko la ajira kwenda sambana na dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Kwa upande wa Rais wa IYF ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw.William Reese alisema mfuko wao umeandaa mpango huo kwa nchi za Tanzania na Msumbiji kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na uujasirimali.

“Tatizo la ajira siyo la Tanzania tu bali la dunia nzima kwa nchi zilizoendelea na ambazo hazijaendelea”, na hitaji mipango ya pamoja, ya kidunia na yakinchi  kwa kushitrikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali” alisema Bw. Reese.

Pia  Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika IYF (Regional Director,Africa) , Bw.Mathew Breman alisema mpango wa jiandallie ajira utaendeshwa kwa muda wa miaka mitano na unalenga kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na jasirimali kwa  vijana.

” Programu hii inahusu vijana wa miaka 18 hadi 24 na watapata mafunzo na mikoa inayolengwa ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara,na Morogoro,” na  vijana 22,500 watanufaika na mradi huu, aliongeza Bw. Breman.

Aidha Bw. Breman mradi unaletekezwa katika nchi  Msumbiji ambapo kwa pamoja na Tanzania utanufaisha vijana 30,000 kupata mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali katika kipindi hicho.   

Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),Bi. Issa Beng’I alisema program hiyo ni muhimu kwa vijana.

“Tunazo program nyingi hapa nchini Tanzania, ikiwemo  kijana jiajiri, vijana wa bodaboda,vijana wa JKT, na sasa program ya jiandalie ajira itawawezesha kujitambua zaidi,” na kufanikiwa kwa hili ni ukombozi mkubwa kwa taiafa letu, aliongeza kusema Bi. Issa.

Moja ya vijana , Nuru Mungi akitoa ushuhuda wa biashara yake, alisema mafanikio aliyoyapata katika ujasirimali yamekuja baada ya kupata mafunzo  (TECC).

 “ Kutokana na mafunzo haya sasa namiliki kiwanda kidogo cha kutengneza sabuni na naamini kupitia program ya jiandalie ajira vijana wengi  watanufaika na kupanua wigo wa ujasirimali.alisema.


No comments

Powered by Blogger.