Header Ads

WLAC wazindua awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ Jijini Dar es Salaam

 Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), wakikata utepe kuzindua rasmi Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jacckline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally.

 Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni (kushoto) na Jackline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam, kwa pamoja wakiinua vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ iliyofanyika kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, leo. 

 Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

 Sehemu ya wadau na mashuhuda waliohudhuria uzinduzi huo.

 Specioza Sylvester, mkazi wa jijini Mwanza akitoa ushuhuda wa Ukatili jinsi alivyomwagiwa Tindikali na vijana waliotumwa na mumewe kwa ajili ya mali.

 Rukia Hamis, mkazi wa Mbagala Kijichi, akitoa ushuhuda jinsi alivyokatwa mkono na mumewe.

 Rukia akiuvaa mkono wake wa bandia baaada ya kutoa ushuhuda.

No comments

Powered by Blogger.