Header Ads

Halmashauri za UVINZA na BUHIGWE zapewa Mafunzo ya Mradi wa PS3

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kihoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza leo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa watendaji wa halamshauri mbili za Buhigwe na Uvinza ambazo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Misaada la Kimataifa (USAID).

Kanali Gaguti aliwataka watumishi hao wa halmashauri hizo mbili kuchukulia fursa hiyo ya kuanza utekelezaji wa ,radi huo kwa umuhimu kubwa kwani kuanza kwao ni kutokana na changamoto zilizipo katika Halmashauri zao.

"Tutumie fursa hii kikamilifu ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika halmashauri zetu, tumeona kuwa tuna miradi mingi katika maeneo yetu lakini hatuitumii vizuri kutusaidia hivyo tuanze mradi huu wa PS3 kwa kumbukumbu kwa kupiga hatua nzuri ili tuondoke hapa tulipo katika changamoto,"alisema Kanali Gaguti.

 Washiriki wa kutoka Halmashauri za Uvinza na Buhigwe wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe.

Mwanasheria wa Kigoma Grace Letawo akifuatilia mijadala.

 Mijada katika makundi ilianza kwa ajili ya utambuzi wa wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri. 

 Washiriki kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Buhigwe, wakiwa katika mjadala wa kundi lao.

 Mtaalam wa masuala ya uongozi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) akifafanua jambo.

No comments

Powered by Blogger.