Header Ads

BURIANI ; Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wauaga Mwili wa JOSEPH SENGA

 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akifuatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Annastazia Wambura, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, marehemu Joseph Senga, Sinza Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda kwao wilayani Kwimba, Mwanza kwa mazishi kesho.

 Waombolezaji wakiiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda wilayani Kwimba kwa mazishi.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Joseph Senga.

 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akitoa heshima za mwisho.

  Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Joseph Senga.

 Mjane wa marehemu Senga, Winfrida Senga akiuaga mwili wa mumewe.

 Mtoto wa marehemu Joseph Senga, Esther akiuaga mwili wa marehemu babake.

 Mtoto Kapama Senga akisaidiwa alipokuwa akiuaga mwili wa babake.

 Mwakilishi wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania, Seleman Mpochi akitoa salamu za rambirambi pamoja na kuwasilisha mchango uliochangwa na wapigapicha kusaidia shughuli za mazishi za aliyekuwa mpiga picha mwenzao, marehemu Joseph Senga.


 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akijdiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

 Lowassa akiwa na Nape Nauye pamoja na Freeman Mbowe.

 Familia ya marehemu Senga.

 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika akitoa salamu za chama hicho.

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi.

 Waombolezaji wakiwa katika shughuli hizo.

 Freeman Mbowe ambaye ni mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, akielezea pengo lililoachwa na marehemu Senga katika gaezeti hilo pamoja na Chadema.

 Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi za serikali wakati wa kuuga mwili wa marehemu Senga.

 Nape akipeana mkono na Lowassa baada ya kutoa salam za rambi rambi.

 Nape akiteta jambo na Mbowe.

 Mbunge wa Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba, Richard Ndassa, ambaye amewahi fanya kazi na marehemu Senga gazeti la Mfanyakazi, akiuaga mwili wa marehemu Senga.

 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia Chadema, Mgeja akiauaga mwili wa marehemu Senga.

 Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Senga.

 Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa akitoa heshima za mwisho  wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Senga.

 Mpiga Picha wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia amewahi kufanya kazi na marehemu Senga katika gazeti la Mfanyakazi, Deus Mhagale akiuaga mwili wa marehemu Senga.

 Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda, ambaye pia amewahi fanya kazi na marehemu Joseph Senga gazeti la Mfanyakazi akiuaga mwili wa marehemu.

 Waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiuaga mwili wa marehemu Senga.

 Wafanyakazi wa Gazeti la Tanzania Daima waliokuwa wana fanyakazi na marehemu Senga wakiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa Senga.

 Wapiga picha wakiuingiza kwenye gari mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao, marehemu Senga.


Baadhi ya wadau waliokuwa miongoni mwa waombolezaji. Kutoka kushoto ni, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkuru,  Muhidin Sufiani,Rukia Mtingwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanania, Jackson Mmbando.

No comments

Powered by Blogger.