Header Ads

Mahakama Kuu Kanda ya IRINGA imemtia Hatiani Muuaji wa DAUDI MWANGOSI

 Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauaji  kufikishwa.
 Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo.

 Mtuhumiwa wa  mauwaji  ya  Mwangosi  akipakiwa  kwenye  gari  za  FFU.

 Msafala  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiz askari  mwenzao anayekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia  leo.

 Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo.

 Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo.
  

wakili  kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo.

wakili  kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo.

 Siku ambayo  mwanahabari  Daudi  Mwangosi  alipouwawa.

 Askari  hao   wakimtoa mahakamani  hapo  leo  mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi.

                               
Marehemu  Mwangosi  enzi  za uhai  wake. 



MAHAKAMA   kuu  kanda  ya  Iringa   imemtia hatiani   kwa   kosa la  kuua bila  kukusudia  askari  Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa  G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa  kuuua  mwaahabari  Daudi  Mwangosi   mwaka 2012 katika  kijiji  cha  Nyololo  wilaya ya  Mufindi.

Huku   wakili  upande  wa jamhuri  katika  kesi  hiyo  Adolph Mwaganda akiiomba  mahakama   hiyo  kutoa   hukumu  ya  kifungo  cha maisha  jela  kwa askari  huyo ambae  hata   hivyo  alisema upande wa  jamhuri  hauna  taarifa  za  makosa yoyote  aliyopata  kuyafanya.


Hata   hivyo  mahakamani  hiyo  imesema  adhabu  kwa  mtuhumiwa   huyo  kutokana  na kupatikana na  kosa  hilo la  kuua bila  kukusudia  itatolewa  Julai 27  majira ya  saa 4  asubuhi  mwaka   huu.


 Jaji  Dkt  Paul Kiwelo ambaye  anayesikiliza  kesi  hiyo alisema  mahakakamani hapo leo    kuwa kati  ya  vielelezo  vitano vyote  vilivyoleta  kama  ushahidi  mahakamani  hapo  kwa ajili ya  kesi   hiyo  namba 54 ya  mwaka 2013  ni  kielelezo   kimoja  pekee  cha  ungamo  kwa  mlinzi  wa amani  ambacho  ndicho  hakukuwa na  shaka   na ungamo  hilo  ndilo  lililomtia hatiani  asikari  huyo.


Alivitaja   vielelezo vilivyopelekwa kama  ushahidi   kuwa ni Ramani   ya  eneo la  tukio,ripoti  ya  tabibu ,ungamo  la mlinzi  wa amani ,silaha  aliyoitumia  na  rejista  ya  silaha  .


Hata  hivyo  alisema  kuwa  idadi  ya   mashahidi  katika   kesi sio  inayowezesha  kumtia  hatiani  mtuhumiwa  ila  kinachomtia  hatiani  ni aina ya  ushahidi wenye  uhakika ambao  unatolewa na  kuongeza  kuwa katika   kesi  hiyo  upande  wa  jamhuri  ulishindwa  kuleta mashahidi  stahiki zaidi ya  kuwa na mashahidi  ambao ukiacha mlinzi wa amani mashahidi wote  ushahidi   wao una masahaka na  haoonyeshi kama mtuhumiwa  huyo  ndio  aliyehusika na mauwaji .


“ Niseme baada  ya   kusikiliza  ushahidi  wote …..mtuhumiwa kaonekana na kosa la  kuua   ila kujua kama  alikuwa na  nia ovu ama bila  kukusudia  ni jukumu la Jamhuri  ambayo  ilipaswa kuleta  ushahidi ….. maelezo  ya  ungamo ambayo  hata  hivyo hayaonyeshi alipanga  ila ni  uzembe  wa hali ya  juu …..haijathibitika kuwa alikusudia mahakama  inaamini  hakukusudia”


Hivyo  alisema  kuwa mahakama  yake imelifuta  kosa  la  kuua kwa  kukusudia  na  kumtia  hatiani  kwa  kosa la  kuua bila   kukusudia alisema     jaji  Kiwele kuwa  hamakama  yake inashangazwa na RCO  kwa   kuleta  mahakamani kesi  ambayo ushahidi  wake  haukukamilika .


“ Ushahidi  pekee  ambao   ni  ule  wa mlizi wa amani hakimu Flora  Mhelela ambae  kweli  alitoa  ushahidi  usio  na shaka  hata  kidogo  ila  ushahidi  mwingine   wote ulikuwa na mashaka  mengi mfano  ushahidi  namba  moja , mbili  na  nne  ni  ushahidi  ambao  haukuwa halisi “.


Alisema mfano  jambo la  kujiuliuza katika ungamo  lake  mtuhumiwa  lisema kuwa  silaha  aliyokuwa  akitumika wakati amemzingira  mwanahabari   huyo    ilifyatuka bahati  mbaya  hivyo  ilikuwa ni mbovu  ila  cha  kushangaza hakuna hakuna ushahidi  unaoonyesha  kuwa silaha  hiyo  ilikuwa  mbovu ama nzima.


Alisema  kuwa  si salama sana  kumtia hatiani  mtuhumiwa   huyo  kwa  kosa la mauwaji  ya  kukusudia  wakati upande  wa jamhuri  umeshindwa   kuleta  ushahidi kamili  unaoonyesha  kuwa mtuhumiwa   huyo  alikusudia   kufanya mauwaji  hayo.


Aidha  alisema  mbali ya  upande  wa  utetezi   pamoja na mtuhumiwa  kukana ungamo  alilolitoa  Septemba 5  mwaka 2012  kwa mlinzi  wa amani  kuwa hakulitoa  kwa uhuru na amani ila bado haisaidii  kulikataa sasa  maana  kama si kweli alipaswa  kielelezo   hicho  kukataliwa siku ya  kwanza  kilipofikishwa mahakamani hapo kama  ushahidi hivyo  mahakama  hainashaka  na kieelezo  hicho  amacho  ni  ungamo  kwa mlinzi  wa amani.


Simon ambae  anatetewa  na wakili  wake  Lwezaula Kaijage aliiomba  mahakama   hiyo  kutoa  adhabu  sahihi yenye  jicho  la  huruma  kwa  mteja  wake   huyo kwani hana  wazazi  na  yeye  ndio anategemewa na  wadogo  zake  watano  pia ana mtoto  wa  miaka mitano anayehitaji  zaidi malezi  yake  katika makuzi  yake.



“Mheshimiwa  jaji  huyu  mshitakiwa ni  kijana mdogo  mwenye  miaka 27  na ni  nguvu kazi ya  Taifa  pia katika oparesheni   hiyo  ya  Septemba 2 mwaka 2012 alikuwa katika kazi  hiyo ambayo  ilikuwa ni amri ya jeshi  na kuwa  slaha  ililipuka  bahati  mbaya  basi  ijulikane    hivyo  pia  amekuwa mahabusi  miaka minne na kwa  kipindi  chote  amekuwa akijutia  kosa lake hilo…. Naomba  anachiwe  huru  kwa masharti  ambayo mahakama inaona  yanafaa”.



Huku   wakili  upande  wa jamhuri  katika  kesi  hiyo  Adolph Mwaganda akiiomba  mahakama   hiyo  kutoa   hukumu  ya  kifungo  cha maisha  jela  kwa askari  huyo ambae  hata   hivyo  alisema upande wa  jamhuri  hauna  taarifa  za  makosa yoyote  aliyopata  kuyafanya.


“ Hatuna  kumbukumbu ya kosa   lolote  ila  kwa  kuwa  mahakama  imemtia  hatiani kwa  kosa  dogo la kuua  bila   kukusudia  tunaomba  mahakama  yako kutoa adhabu  kwa  mujibu wa  kifungu  namba 198cha  kanuni  ya adhabu  sura  namba 16 mapitio  ya  mwaka 2002 kwamba  mtu  yeyote aliyetiwa hatiani  kwa  kosa la  mauwaji   ya  bila  kukusudia  afungwe  jela  maisha “


Kesi   hiyo ambayo ilijaza  umati  mkubwa wa wakazi wa mji  wa Iringa  huku  polisi  wa FFU  na  wale  wa kawaida wakitanda  nje  ya  mahakama  hiyo  na ndani ya  chumba  cha mahakama  kabla ya  msajili wa mahakama   hiyo  kutoa onyo  kwa  jeshi  la  polisi kufuatia  vurugu  mbali  mbali  wanazozifanya mara kwa mara  katika  kesi   hiyo , wakili  kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  alisema  kuwa  hajapendezwa na  nguvu  kubwa ya   jeshi  la  polisi ambayo wanaitumika katika  kasi   hiyo  ndani  na nje  ya  mahakama  kuwa  kinachofanyika ni  kuingilia uhuru  wa mahakama.


Kwani  alisema mahakama  haipaswi  kuingiliwa na chombo  kingine   chochote   na kuwa  kitendo  cha  polisi kuzuia  wanahabari ndani  ya mahakama  kufanya kazi zao kabla ya  kesi  kuanza ama  baada ya  kesi  kumalizika  si haki .

Lakini pia wakili msom I Ishabakaki, alisema  kwa maoni yake anaona kulikuwa na mapungufu kwanzia kweye uchugunzi wa kesi ya mpaka uendeshaji wa kesi hiyo. Wakili msomi alisema anaunga mkono maswali ambayo mahakama ilijiuliza kwa nini RPC na RCO  hawakuitwa kutoa ushaidi.

 Wakili anasema kutkana na mwenendo wa kesi   kwa  kitendo cha viongozi wa juu kutokuita mahaakamani kuisaidia mahakama kunaweza kukawa kumepindisha haki sit u kwa marehumu mwangosi lakini  hata kwa askari aliyehukuiwa. 

Hii ni kutokana na kwamba mahakma iisema imepata kazi sana kutambua siku hiyo oda ilitoka kwa nani.

No comments

Powered by Blogger.