Header Ads

Alichokizungumza Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA katika Ziara yake ya LINDI na MTWARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa  ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya  za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi.  Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016. 
LIO2 

Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.

 “Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.

“Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha.

LIO3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja uliopo kwenye kata ya  Nachingwea mjini Ruangwa Julai 16, 2016. 

LIO4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi  , Renather Mzinga ambaye amepandishwa cheo na kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi. Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 16,2016.

LIO5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi, viongozi na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. 
LIO6 
Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. 
LIO7 
Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016.  

No comments

Powered by Blogger.