Header Ads

Washindi wa Mbio za Baiskeli Kanda ya Ziwa Wakabidhiwa Zawadi Zao

  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli.

  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa meza kuu kwa ajili ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo. 

Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Seni Konda akifurahia zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.
Mshindi wa pili katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Makoja Hamis akionesha  zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa Mashindano hayo ya baiskeli, Hamis Clement.

Washindi kwa upande wa wananume wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Na Dixon Busagaga

FAINALI ya mashindano ya mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle challange 2016 zinazoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za baiskeli (CHABATA) na kudhaminiwa na kampuni ya kuchimba Madini ya Acacia zimemalizika mjini Kahama huku mwendesha baiskeli Seni Konda akiweka rekodi ya kushinda mbio hizo kwa kutumia saa 4:15:07 .

Konda mkazi wa mkoa wa Shinyanga amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wake Makoja Hamis aliyemaliza nafasi ya pili na Hamis Clement aliyemaliza nafasi ya tatu huku wakifuatiwa na waendesha baiskeli zaidi ya 150 walioshiriki mbio hizo kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa.

Kwa upande wa wanawake ,mwendesha baiskeli,Martha Anthony kutoka mkoani Mwanza amefanikiwa kutetea ubingwa wake akimaliza wa kwanza huku akiwashinda washindani wake,Salma William aliyeshika nafasi ya pili na Elizabeth Clement aliyeshika nafasi ya tatu.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ,Seni Konda amejinyakulia kitita cha sh Mil 1.5 ,mshindi wa pili Makoja Hamis akijinyakulia kiasi cha sh Mil moja huku mshindi wa tatu ,Hamis Clement akiambulia kiasi cha sh 700,000.

Upande wan wanawake mshindi wa kwanza Martha Anhtony amejinyakulia kiasi cha sh Mil 1.2,mshindi wa pili Salma William akipata sh 800,000 huku mshindi wa tatu ,Elizabeth Clement akipata sh 600,000.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo mgeni rasmi naibu waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Anastazia Wambura amesema michezo ni ajira na afya ambapo pia amewataka wachezaji kutotumia madawa ya kusisimua misuri kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za michezo na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli cha Tanzania (CHABATA) Jacx Mhagama alisema  CHABATA na kampuni ya madini ya ACACIA wamesaini mkataba wa udhamini wa mashindano hayo  kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2014 mpaka 2016.

“Kipindi hiki cha miaka mitatu kimekuwa na mengi kiutendaji na kimahusiano kwetu sote CHABATA na ACACIA. lakini kwetu imekuwa ni kipindi chenye chenye changamoto zenye kutukomaza na kutujenga.  Hivyo tumevuna tuliyoyategemea na ziada pia.”alisema Mhagama.

 “ACACIA ni kampuni yenye machimbo ya madini kwenye eneo hili la kanda ya Ziwa, lakini wameonyesha upendo na uzalendo mkubwa hata kwa Taifa. Pamoja na kujishughulisha na michezo kwenye eneo hili la kanda ya ziwa, wameenda juu Zaidi kufikia taifa kwa kuifadhili timu yetu ya Taifa ya Baiskeli kwenye mashindano ya Ubingwa wa Afrika mwaka jana 2015, yaliyofanyika huko Petermarizburg nchini Afrika ya Kusinu.”aliongeza Mhagama.

No comments

Powered by Blogger.