Header Ads

Mwenyekiti Dkt JAKAYA KIKWETE aongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mjini Dodoma



 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli akiteta na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar,  Dkt. Ali Mohamed Shein katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba  wimbo wa CCM katika kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016. 
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments

Powered by Blogger.