Header Ads

Mwili wa Mwanahabari JOSEPH SENGA wawasili Nchini Ukitokea INDIA

 Waombolezaji miongoni mwao wakiwemo waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa MpigaPicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaamm jana, ktuoka nchini India ambako alipatwa na mauti, Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia alifika kwenye mapokezi hayo. 

 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Senga wakiwa Uwanja wa Ndege wakisubiri wa mpendwa wao.

 Maofisa wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Uwanja wa Ndege, Swisport wakitoa nje jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga.

 Waombolezaji wakiuweka mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa Hos[pitali ya Muhimbili.

 Wanachama wa Press Photographers Tanzania wakishiriki kuingiza kwenye gari jeneza la mwili wa wa aliyekuwa mpiga picha za habari Tanzania, marehemu Senga.

 Dada wa marehemu Joseph Senga, Yunista Senga akilia kwa uchungu alipoona jeneza lenye mwili wa kaka yake, Joseph Senga.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akielezea kwa masikitiko kuhusu msiba wa Joseph Senga.

 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wapigapicha za habari wakiondoka Uwanja wa Ndege baada ya kuupokea mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao.


No comments

Powered by Blogger.