Header Ads

Waendesha Baiskeli Zaidi ya 150 Wachuana Katika "TUFANIKIWE PAMOJA CYCLE CHALLENGE 2016"

 Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha baiskeli.

 Waendesha baiskeli kutoka mikoa sita ya kanda ya Ziwa wakijiandaa kuchuana wakati wa Mashindano ya mbio za baiskeli ya Acacia Tufankiwe Pamoja Cycle Challenge 2016 yaliyofanyika mkoani Shinyanga chini ya yakidhaminiwa na kampuni ya Madini ya Acacia .  

  Baadhi ya Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakitafakari kabla ya kuanza kwa mbio hizo.

 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo akizungumza jambo na Mgeni Rasmi ,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura kabla ya kuanza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.


 Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Baiskeli Tanzania (CHABATA) Godfrey Mhagama akieleza sheria mbalimbali za mchezo huo kabla ya kuanza rasmi mbio hizo.

 Asa Mwaipopo ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ulio chini ya Kampuni ya Acacia ,akizungumza kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.Wengine kutoka kulia ni  
Meneja Uendelevu wa Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Buzwagi,George Mkanza,Mgeni rasmi katika mashindano hayo Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura na katikati ni Katibu wa Baraza la Michezo (BMT) ,Said Kiganja. 

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akivishwa kofia ngumu kabla ya kufungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016. 


Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura akiendesha baiskeli kuashiria kufunguliwa rasmi kwa mashindaano ya Acacia Tufanikiwe Pamoja  Cycle Challange 2016.

Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa ameshika bendera ,tayari kuanzisha  mbio hizo,kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.

Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakianza mbio hizo.

Washiriki wa Mbio hizo wakipita katika eneo la Kagongwa Kahama.

Muonekano wa picha ya juu eneo la Phantom eneo  ambako mashindano hayo yalianzia na kumalizikia.

Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle  Challange 2016 wakihitimisha mbio hizo.

No comments

Powered by Blogger.