Header Ads

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA akabidhiwa Madawati ya Shule za Dar es Salaam

aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo kukbidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salaam  Julai 28, 2016.Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke  Felix Lyaviva.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , Balozi Augustine Mahiga (kulia kwake) wakifurahi  wakati , Bwana Murtaza Adamjee alipoongoza wimbo katika hafala ya kukabidhi madawati kwa mkoa wa Dar es salaam iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.

No comments

Powered by Blogger.