Shilingi Bilioni 21 Zimetengwa Ujenzi wa Meli Mpya Ziwa Victoria
Serikali imetengaTsh. Bilioni
21 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria katika Mwaka wa
Fedha 2016/17 ili kutekeleza ahadi iliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ya kuondoa adha ya usafiri katika ziwa hilo.
Hayo yamesemwa leo Bungeni
Dodoma na Naibu wWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Edwin
Ngonyani wakati akijibu swali la mbungewaUkerewe (CHADEMA), Mhe. Joseph
Michael Mkundi aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuleta meli mpya
katika Ziwa Victoria.
“Serikali ina mipango thabiti
ya kujenga meli mpya zitakazotoa huduma ya usafiri na usafirishaji
katika Ziwa Victoria na maziwa mengine makuu ya Tanganyika na
Nyasa,”alisema Ngonyani.
Kuhusu ukarabati wa meli ya MV Butiama iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Bandari za Mwanza na Nansio Ukerewe, Ngonyani
alisema tathmini ya uharibifu ilibaini kuwa injini iliharibika sana na
isingefaa tena kutumika kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.
Aidha, Ngonyani alisema ilibidi
inunuliwe injini nyingine mpya pamoja na gia boksi yake na kuongeza
kuwa tayari Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ilikamilisha mchakato wa
kupata injini stahiki kwa ajili yamelihiyo kwa beielekezi.
Ngonyani alisema kuwa katika
Mwaka wa Fedha wa 2016/17 serikali kupitia MSCL imetenga Tsh. Bilioni
3.6 kwa ajili ya matengenezo ya meliya MV Butiama ambayo yanataraji
kukamilika ndani ya miezi kumi.
Kwa mujibu wa Ngonyani, MV
Butiama ilisItisha huduma ya usafiri kati ya Mwanza na Nansio, Ukerewe
mwaka 2010 baada ya injini yake kupata uharibifu mkubwa wa kukatika
mhimili wake (Cranshaft).
Kwa upande wake Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi
kuhusu ukarabati wa Meli ya MV Liemba alisema mazungumzo yanaendelea na
Serikali ya Ujerumani kuikarabati meli hiyo ambayo imefanya kazi kwa
miaka zaidi ya mia moja.
Post a Comment