SERIKALI kutoa Vifaa Tiba kwa Wajawazito 500,000 hapa Nchini
SERIKALI katika mwaka 2016/17
imekusuduia kutoa vifaa vya kujifungulia kwa wanawake wajawazito 500,000
ili kuwasaidia kukabiliana na matatizo ya uzazi pingamizi ikiwemo
ugonjwa wa Fistula.
Hatua hiyo imekusudiwa
kuchochea na kuwahamasisha wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo
vya huduma ya afya nchini badala ya kufika kwa wakunga wa jadi.
Hayo yamebainishwa leo Bungeni
mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa
Viti Maalum (CCM), Mgeni Jadi Kadika.
Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.
Waziri Ummy alisema ugonjwa wa
fistula umekuwa ukiwapata wanawake wa hadhi ya chini hususani wale wa
vijijini ambapo kuna uhaba wa miundombinu ya vituo vya afya, uhaba wa
wataalam na msongamano wa wa kupata huduma.
Waziri Ummy alisema ugonjwa wa
fistula hausababishwi na kurogwa, laana au kutembea na wanaume wengi,
kama ambavyo baadhi ya wanajamii wanavyoelewa, hivyo ili kukabiliana na
uginjwa huo Serikali imekuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhamasisha
wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.
“Tutawahamisha wanawake wote
wajawazito hususani wa kiuanzia miezi 2 na kuendelea wanaanza kliniki
mapema ili kuwasadia na uzazi pingamizi,” alisema Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema
Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa hospitali za rufaa za mikoa
nchini zinakuwa na huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wa fistula ili
kuwawezesha wanawake wenye tatizo hilo wanapata huduma za matibabu kwa
ufanisi.
Alisema ugonjwa wa fistula
umekuwa na madhara ya kijamii, kiafya na kiuchumi ikiwemo wajawazito
wengi kupoteza watoto, wanawake kuachwa na waume zao pamoja na akina
mama hao kushindwa kujihusisha shughuli za maendeleo.
Post a Comment