Baadhi
ya waandishi wa habari wakiangalia video ya faida za vitambulisho vya Taifa
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya
kuelimisha umma kwenye mkutano wa Mamlaka hiyo na waandishi wa habari
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
“Upatikanaji wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali
kuondokana na tatizo la Watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na
mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma” alisisitizaMdami.
Utoaji huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za
utambulisho kwa wananchi ilizisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati
mchakato wa kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.
Mdami alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili
ya uhakiki wa taarifa hizo.
Lengo la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni kuhakikisha
kuwa ifikapo Desemba mwaka huu wananchi wote wawe wamepatiwa namba ya
utambulisho .
Picha
na Fatma Salum (MAELEZO)
|
Post a Comment