Header Ads

Timu Zinazoshiriki Michuano ya "SPORTS XTRA NDONDO CUP" zakabidhiwa Vifaa vya Michezo

NA RAYMOND URIO
Timu 32 zinazoshiriki ligi ya Michuano ya Dr MWaka Ndondo Cup za jijini Dar es SAlaam, zimekabidhiwa vifaa leo katika ukumbi wa Escape uliopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwaka wa Tatu sasa tangu Michuano hiyo ilipoanza chini ya Waandaji Clouds Media Group  kwa kushirikiana na DRFA ambao ni chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Uhusiano wa Kliniki ya Foreplan, Baraka Samwel Mgeyuka (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari na vilabu vilivyofuzu katika mashindano ya Dk Mwaka Ndondo Cup hatua ya 32 bora yaliyoapngwa kuanza Jumapili. Katikati ni Mkurugenzi wa Kliniki hiyo, Tully Mwaka na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo. 

(Picha zote na Raymond Urio)

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwakilishi wa Clouds Media Group, Shaffi Dauda, amesema kuwa michuano hiyo imefikia hatua ya MAkundi baada ya kumalizika mzunguko na ambapo jumla ya timu 16 zilifanikiwa kuingia hatua hiyo toka mwaka jana na timu zilizobaki pia zimeweza kuingia hatua hiyo baada ya kupambana kwa udi na Uvumba hadi kufanikiwa kupata nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa Michuano hiyo na utoaji wa Vifaa vya Ligi ya Dkt. Mwaka Ndondo Cup.

 Jumla ya vifaa vyenye tahamani ya Milioni 40 zimekabidhiwa ikiwa ni pamoja na Jezi full kwa timu zote shiriki, jezi za waamuzi na na jezi za makipa kwa timu zote, ambapo msemaji wa foreplan Clinic BAraka Samweli, wamesema kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa MAra mbili ukilinganishwa na michuano ya miaka miwili iliyopita, ambapo pia imeongezeka kwa Kikundi cha Ushangiliaji.


 Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kliniki ya Foreplan Clinic, Tully Mwaka (kuli),akikabidhi mpira kwa kiongozi wa timu ya Madiba FC ya Segerea, Dennis Rocky wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa kwa timu 32 zilizofuzu hatua ya 42 bora ya mashindano ya Ndondo Cup.
 
 panda kutoka Milioni Tano na kufikia Milioni 10, ambapo pia amewataka washiriki wa michuano hiyo kuyatumia mashindano hayo kwa nidhamu ili kuleta tija ya kuokoa vijana wengi katika kukuza Vipaji kwa vijana wa jiji la Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Kliniki ya Foreplan, Baraka Samwel Mgeyuka (katikati) akiziangalia baadhi ya jezi watakazo pewa baadhi ya timu zitakazo shiriki katika Ligi hiyo ya Dkt. Mwaka Ndondo Cup, Kushoto ni Mwenyekiti na Chama cha Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo, na Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Kanuti. 

MWenyekiti wa chama cha Mpira wa Mkoa wa Dar es SAlaam kama mwakilishi wa kamati ya mashindano bwana almasi KAsongo amesema kuwa anajivunia na kufarijika kutokana na kuwajumuisha makundi mbalimbali baina ya Wachezaji wa timu, Viongozi, Vyama vya Soka na Waandishi wa habari ambapo Faida kubwa imeendelea kupatikana ikiwa ni baada ya timu za Ligi kuu ya Tanzania na Ligi zingine kujikuta ikiwatumia wachezaji wengi wanaoshiriki kwenye hii michuano ya DR MWAKA NDONDO CUP.

Pamoja na kushiriki mwaka wa tatu hadi sasa michuano hiyo aijaingia kwenye dosari yoyote kama zilivyo ligi zingine ambapo mara nyingi wachezaji wanafikia wakati mwingine kushikana mashari, ugomvi pamoja na kuharibu sifa za mashindano imekuwa tofauti sana na michuano hii.

Kwa upande mwingine Shaffi Dauda kutoka Clouds MEdia Group amesema Changamoto kubwa iliyoonekana kwenye michuano hiyo kwa mwaka jana ni baadhi ya timu ususani mashabiki kujazana kwenye eneo la wachezaji ambapo kwa mwaka huu wametakiwa mashabiki wote kutojihusisha na eneo la Timu zinazoshiriki na kuwaacha wachezaji eneo husika kwa ajili ya usalama wa timu na wachezaji.

No comments

Powered by Blogger.