Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI akagua Ujenzi wa Kituo cha Kufua Umeme cha KINYEREZI II

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akianza ukaguzi katika Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kinyerezi hawapo pichani kabla ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba akifafanua jinsi ujenzi wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II kitakavyokuwa mara baada ya kukamilika  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia huko Kinyerezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU

No comments

Powered by Blogger.