Header Ads

Naibu Waziri ABDALLAH POSSI atembelea Shule na Vituo vya Watu wenye Ulemavu Mkoani MANYARA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na wanafunzi na uongozi wa shule ya msingi Katesh “A” na “B” (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara shuleni hapo ili kuona hali ilivyo katika kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum, Machi 2, 2016.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na watoto wenye ualbino wanaolelewa na kituo cha 4 Angle Disabled Children kilichopo Wilaya ya Haydom Mkoani Manyara wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo, shule na vyuo vya watu wenye ulemavu. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa na Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha 4 Angle Disabled Children kilichopo Wilaya ya Haydom Mkoani Manyara wakati wa ziara yake kituoni hapo.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments

Powered by Blogger.