Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wialaya ya Kigamboni Januari 3, 2016.
..................................
Waziri mkuu
wa Tanzania KASSIM MAJALIWA amefuta posho za vitafunwa na zile zisizokuwa kwa
mujibu wa sheria katika vikao mbalimbali vya Halmashihauri na kuagiza fedha
hizo kutumika katika shughuli za maendeleo.
Waziri mkuu
ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kigamboni jijiji Dar es
salaaam kukagua shughuli za maendeleo akiambatana na watendaji mbalimbali wa
serikali.
MAJALIWA
amewatahadharishwa wakurugenzi wa manispaa watakaopitisha fedha hizo na kueleza
kuwa watachukuliwa hatua kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa.
Mapema
akizungumza na watumishi wa wilaya mpya ya kigamboni,Waziri mkuu ametoa siku
tatu kwa watumishi 10 waliohamishiwa Wilaya
kigamboni na hadi sasa hawajaripoti katika vituo vyao vya kazi kuripoti mara
moja.
Akiwa katika
moja ya kiwanda cha kuzalisha maziwa kata ya Kisarawe Two, Waziri MAJALIWA
ameeleza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa
viwanda.
Katika ziara
hiyo waziri mkuu ametembelea ujenzi wa wodi ya wazazi kata ya Kisarawe Two
kisha kumaliza ziara yake katika kiwanda cha uzalishaji maziwa kilichopo
kisarawe two na kukagua shughuli za uzalishaji.
|
Post a Comment