Na Sheila Simba-MAELEZO
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.
Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.
|
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na
wakandarasi nchini na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili
kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.
“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.
|
|
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof
Makame Mbarawa akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kumi na Nne wa Bodi ya
Wahandisi nchini leo JIjini Dar es Salaam, ambapo aliahidi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa wakandarasi nchini katika kutimiza majukumu yao. |
|
wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu
Lema (katikati) akimkabidhi Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli hundi ya shilingi milioni Miamoja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa
vya maabara katika shule za sekondari nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.
akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.
“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda.
|
|
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya pamoja na wakandarasi waliohudhuria mkutano huo.
|
Post a Comment