Mbunge wa Segerea BONNAH KALUWA aongoza Semina ya Wanawake Wajasiriamali
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa
(katikati) akiingia kwenye ukumbi wa Nyantale kwa ajili ya kufungua semina ya
ujasiriamali ya wanawake eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya
ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya
ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Ofisi ya Jimbo la
Segerea,Jacqueline,akizungumza na akinamama wa jimbo hilo kwenye semina ya
ujasiriamali.
Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya
Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa
mapato na matumizi jinsi inavyosaidia kwa wajasiriamali kukua kibiashara kwenye
semina hiyo.
Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF,Erica Sendegeya,akizungumza na wanawake wajasiriamali umuhimu na faida ya
kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye semina hiyo.
Mkufunzi wa Kujitegemea,Albert Magonga,akitoa mojawapo ya mada ya kuwawezesha
wanawake wajasiriamali kukua kiuchumi kupitia biashara zao.
Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka
Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio
wa mapato.
Mama mjasiriamali akichangia mada katika semina hiyo.
Semina ikiendelea....
Wanawake wajasiriamali wa Jimbo la Segerea wakisikiliza
kwa makini wakufunzi waliokuwa wakizungumza kwenye semina ya ujasiriamali ya
kuwainua kiuchumi wanawake.
Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo
la Segerea,Salma Fumbwe,akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la
Segerea,Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake
iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo.
Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Na Elisa Shunda
WANAWAKE washauriwa kutenganisha fedha ya msingi wa
biashara na fedha ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ili kuboresha na kusonga
mbele kiuchumi tofauti na wakichanganya watakuwa wanadumaza biashara zao na
matokeo yake kupata hasara inayopelekea kusimamisha biashara anayoifanya.
Hayo yamezungumzwa na wakufunzi mbalimbali waliokuwa
wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake kwenye semina yenye ujumbe wa kauli
mbiu ya Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la
Segerea,Bonnah Kaluwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata
Bima jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza kwenye semina hiyo mbunge wa jimbo
hilo,Bonnah Kaluwa,alisema kuwa ameamua kuandaa semina ya ujasiriamali ya
wanawake kwa ajili ya kuwapatia elimu mbambali za ujasiriamali pamoja na elimu
ya utunzaji wa fedha za biashara kwenye sehemu yenye uhakika pasipokuwa na
shaka wala wizi kwa kuwaletea benki ya Equity na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ya
PPF ambao watawasaidia kuwahifadhia fedha zao pamoja na kuwapatia bima ya afya
na fao la kustaafu endapo watakidhi vigezo.
“Wakinamama nimefurahi kwa jinsi mlivyojitokeza kwenye
semina hii natumaini tukimaliza hapa kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya
kutosha kuhusiana na masuala ya ujasiriamali likiwemo la kutofautisha fedha ya
matumizi ya nyumbani na fedha ya biashara kwa kuwa ukipata elimu ya
kutenganisha vitu hivyo utaendelea kwenye biashara yako huwezi kutoa fedha ya
biashara kununua chakula au kumsomesha mtoto lazima utayumba hivyo ni bora kila
mtu ategeshe sikio lake vizuri kusikiliza elimu itakayotolewa hapa ambayo
itatufumbua kutofautisha masuala ya nyumbani na biashara ambayo itatusaidia
sana kufikia kwenye malengo yetu” Alisema Kaluwa
Aidha akitoa elimu ya ujasiriamali kwenye semina
hiyo,mkufunzi wa kujitegemea,Albert Magonga,alisema kuwa huwezi kuwa
mjasiriamali halafu huweki mazingira ya kuonyesha bidhaa zako kwa majirani yako
wanaokuzunguka na pia ni vyema mjasiriamali kuwa mbunifu wa kutambua eneo
unaloishi ni kitu gani ambacho ni adimu ili uanzishe upate wateja wako ambao
watanunua biashara yako kutokana na jinsi unavyokiandaa.
Naye Mkufunzi wa utunzaji wa fedha kutoka benki ya
Equity,Daudi Mwashilindi,alisema kuwa watu wengi wanaokopa fedha katika taasisi
mbalimbali nchini wana mapungufu ya kutokuwa na elimu ya fedha jinsi ya
kuitumia akatolea mfano benki yao wanakopesha hadi maprofesa ambao wanaaminika
wana upeo mkubwa wa kufikiri lakini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha
wanashindwa kutumia vizuri fedha walizokopa mwisho wanauza nyumba yake ili
kurudisha kiasi cha fedha walizomkopesha.
“Unapotaka kwenda kukopa katika taasisi yoyote ya fedha
ni lazima uwe na elimu ya matumizi ya fedha la sivyo utaishia pabaya kwa mfano
benki yetu ya Equity tunakopesha hadi maprofesa ambao tunaamini wana upeo
mkubwa wa akili ila kutokana na kutokuwa na elimu ya utunzaji na utumiaji wa
fedha wanashindwa kurudisha fedha zetu tunauza nyumba yake kwa ajili ya
kurudisha kiasi cha fedha tulizomkodisha,hivyo ninyi leo mnapata elimu ya kujua
bajeti yako na mapangilio wa mapato na matumaini ikiwemo na daftari la biashara
zako ili kujua mahesabu yako” alisema Mwashilindi.
Akaongeza kwa kusema mjasiriamali bora anapaswa kupata
taarifa sahihi kutoka kwenye vyombo vya habari ni fursa kwake akatolea mfano
ukipata taarifa ya habari kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mwezi wa kumi
kutakuwa na joto kali wewe kama mfanyabiashara kutokana na taarifa hiyo lazima
apange biashara ya kuuza vitu vinavyoendana na kipindi hicho kwa kufanya
biashara kama Soda,Maji na Juice.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Erica Sendegeya,aliwashauri akinamama wajasiriamali kujiunga na
mfuko huo utakaowasaidia mambo mbalimbali ikiwemo la masuala ya afya kwa kupata
vitambulisho vya NHIF kwa bei nafuu na kuwaambia mfuko wa PPF ukichangia kwa
takribani miaka 15 kwa kila mwezi shilingi 20000 unaingizwa kwenye fao la
pensheni hivyo aliwataka wakinamama hao kujiunga na mfuko huo.
Semina hiyo ya ujasiriliamali kwa wanawake wa jimbo la
Segerea itawezesha kuwapatia elimu ya utunzaji wa fedha akinamama zaidi ya 500
ambao wapo kwa kanda mbili ambapo mkutano huu wa mwanzo ulifanyika kwenye jimbo
hilo kwa kanda ya A ambapo baadae kanda B nao watapatiwa elimu hiyo kupitia
ufadhili wa benki ya Equity na Mfuko wa Hifadhi ya jamii kushirikiana na ofisi
ya jimbo la Segerea.
Post a Comment