Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa
ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 leo jijini Dar es
Salaam.
Na Veronica Kazimoto
Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi
trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na
Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa
amesema ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo
kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli hizo zimekuwa kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa
asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi,
Dkt. Chuwa alisema kumekua na ongezeko
la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 11.2
mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza
kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na
kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.
Shughuli za uchukuzi na uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema
kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha asilimia 30.6 zikisababishwa na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli na
barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile, shughuli za fedha na bima zimeongezeka kwa
kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia 10.0 iliyopatikana katika
kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia
8.0 katika robo hiyo ya mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama
hicho kwa mwaka 2015 ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la
wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika
Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi
kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda katika
kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4 ikilinganisha
na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.
Takwimu za Pato la Taifa kwa robo
mwaka hupimwa kwa kutumia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini
katika vipindi vya miezi mitatu mitatu ambavyo ni Januari – Machi, Aprili –
Juni, Julai – Septemba na Oktoba – Desemba ambapo hujumuisha shughuli zote za
kiuchumi, na hutumika katika kutathmini, kupanga mipango na kutayarisha sera za
kiuchumi.
Post a Comment