Mwenge wa Uhuru Wapita Katika Miradi 9 Wilayani IKUNGI
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe akimkabidhi Mwenge wa uhuru mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kulia).
Wananchi wakifatilia kwa karibu makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilayani manyoni kuhamia Wilayani Ikungi.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Lucia vitalis Kamafa kutoka Manyara akiuhifadhi mwenge huo kwenye sehemu yake ya kuhifadhiwa.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wa nne kutoka kushoto.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akisoma Maandishi yanayohimiza kuachana na Rushwa yaliyoandikwa na Klabu ya Rushwa Shule ya Sekondari Mkiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akiwasaidida kina mama kuwatwisha Ndoo kichwani mara baada ya kutembelea Mradi wa Maji wa Rafiki katika kijiji cha Muungano Kata ya Unyahati.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya stendi-Ikungi.
Na
Mathias Canal. Singida
Takribani Kilomita 141.5 zimetumika kukamilisha
ziara ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Ikungi ambapo umepita kwenye Miradi tisa
yenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni 975,991,180.44 kati ya miradi hiyo,
Miradi mitatu imewekwa mawe ya msingi, Mradi mmoja umefunguliwa, Miradi mitano
imezinduliwa, Miradi sita imekamilika sawa naasilimia 67 na miradi mitatu
itakamilika ifikapo June 30, 2017.
Ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 umebeba
ujumbe unaosema “Vijana ni Nguvu kazi ya
Taifa” na kauli mbiu isemayo “Washirikishwe
na Kuwezeshwa” ukiwa umejikita katika kuhimiza dhana ya wananchi kushiriki
shughuli za maendeleo, Usimamizi wa Miradi na pia kuunda Vikundi vitakavyo wawezesha
kukopa na kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima amesema kuwa
Mwenge wa Uhuru ni tunu muhimu kwa Taifa na una lengo la kumulika mahali
kulipokosekana matumaini, upendo na amani na hatimaye kurejeshwa sambamba na kumulika Miradi
mbalimbali ya serikali na watu binafsi ili kuamsha ari ya utendaji uliotukuka
na kurahisisha shughui za maendeleo katika jamii.
Amempongeza Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kubadilisha
kasumba ya utendaji kazi wa mazoea kwa watumishiwa mbalimbali umma na taasisi
za watu binafsi nakurejesha uwajibikaji kwa kila mmoja jambo ambalo limeamsha
ari ya uwajibikaji kwa jamii na watanzania kwa ujumla.
Mbijima
ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kwa
kumbeza Rais kwa utendaji kazi wake jambo ambalo amesema kuwa jambo hilo
littavifanya vyama hivyo kuzidi kupoteza mvuto kwani hiyo ni adhabu ya
udanganyifu mwingi ambao viongozi wa vyamahivyo wamekuwa wakiufanya kwa kipindi
kirefu katika mikutano yao.
Amesema kuwa watanzania wa sasa wanahitaji
uwajibikaji, kukuza uchumi wa kila mmoja mmoja kwa kushirikiana na serikali
hivyo uongo ukizidi bila mafanikio ya utendaji itakuwa sehemu ya kipimo cha
kuwakataa wakati wa kuomba ridhaa tena baada ya miaka mitano ya uongozi wao.
Akisoma risala ya utii ya wananchi wa Wilaya ya
Ikungi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa Mbio za Mwenge wa
uhuru Wilayani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka alisema kuwa Ujumbe
huo wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu kwa vijana unatilia mkazo kwamba maendeleo
hayazuki yenyewe bali jamii kwa pamoja kuwa na kiu na ari ya kufanya kazi ili
iweze kutumika katika kubuni, kupanga na kuweka mikakati inayotekelezeka na
kutekeleza kwa maslahi mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia Hali ya Maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi
huyo alisema kuwa kwa Mwaka 2015 jumla ya watu 8106 sawa na asilimia 56.6%
walipima kwa hiari na jumla ya watu 288 (Wanaume 102 na wanawake 186)
waligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI sawa na asilimia
3.5%,
Kwa mwaka 2016 Januari hadi June jumla ya watu 8158
(Wanaume 3657 na Wanawake 4501) walipima kwa hiari na jumlaya watu 301 (Wanaume
121 na wanawake 180 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI sawa na
asilimia 3.7% na hadi kufikia June 2016 jumla ya watu 2248 (Wanaume 651 na
wanawake 1597) wamesajiliwa kwenye vituo vya Tiba na maangalizi CTC kwa ajili
ya kupata dawa za kufubaza VVU nakati yao jumla watu 1749 sawa na asilimia
77.8% wameanzishwa kupata dawa za kufubazaVVU-ARV (Wanaume 591 na wanawake 1378
sawa na asilimia 86.3%.
Turuka amesema kuwa katika kupambana na VVU/UKIMWI
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi inaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa
wananchi ili kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono kupitia
mikutano ya hadhara, kutoa vipeperushi kwa njia ya mafunzo elekezi, ushauri
wakitaalamu pamoja na kuonyesha Sinema/Video zinazoonyesha maambukiziya VVU na
UKIMWI na jinsi ya kujikinga.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu amesema kuwa
chini ya kauli mbiu “Tujenge jamii yenye afya bila dawa za kulevya” Wilaya yake
inalaani vikali matumizi ya dawa za kulevya na unywaji pombe uliokithiri kwa
kushirikianana wadau na wananchi wote kwa pamoja ili kuondokana na kadhia hiyo
inayoathiri nguvu kaziya Taifa yaani vijana.
Dc Mtaturu alisema kuwa pia Wilaya hiyo kupitia
taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Singida na wadau wake
imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara, vipeperushi na
majarida, Semina na kuunda klabu za
wapinga Rushwa mashuleni na sehemu za kazi ambapo mpaka sasa Wilaya ina klabu
20 za wapinga Rushwa.
Post a Comment