Header Ads

RSM yachangia Madawati 50 katika Mkoa wa Dar es Salaam



RSM, Mtandao wa Kimataifa katika ukaguzi wa mahesabu na tathmini za kodi,  umesherehekea madhimisho  tano ya kila mwaka ya Siku Maalumu Duniani ya RSM—kwa kuchangia madawati kwa shule mbalimbali za Dar es Salaam.
Mchango wa RSM, Mtendaji Mkuu wa RSM Afrika Mashariki, Bi. Lina Rantasi alisema kuwa timu ya RSM imedhamiria kusaidia jitihada za Serikali za kuokoa maisha na kuendeleza elimu.
Bi. Ratansi aliendelea kusema,”Kumekuwa na wito mwingi wa kuchangia madawati, Na sisi hatutaki kubaki nyuma, ndo maana tumetoa madawati 50 (3, 750, 000) ili kusaidia watoto wasika chini tena.”
Amesema madawati utasaidia kuongeza uwezo na akili za watoto katika masomo, hivyo kuongeza ufaulu, kwa sababu “motto akikaa chini hata ufahamu wake unakuwa mdogo.
Akipokea madawati hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati-Mkoa wa Dar es Salaam, Hamid Abdul Rahaman, amesema mchango wa RSM utasaidi kukuza sekta ya elimu, na kuwapongeza Mtandao wa RSM kwa kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.

Background:
hadamu kwani benki ya damu imepungua kiasi cha kutokuwa na damu kabisa. Sisi hapa RSM tumeamua kuchukua hatua na kuwahamasisha wengine kufanya kama hivi. Shime tuungane pamoja kuokoa maisha ya Mtanzania.”
 na sherehe kubwa zaidi za dira na malengo ya pamoja ambayo mtandao huu huru wa sita kwa ukubwa wa ukaguzi, kodi na ushauri wa kitaalamu haujawahi kufanya. Kupitia shughuli za aina mbalimbali duniani kote, wafanyakazi katika mashirika ya RSM zaidi ya nchi 120 zilizounganishwa kwa njia ya mshiriki, mteja na matukio ya hisani katika kusherehekea maadili ya msingi ya RSM ya utendaji kazi wa pamoja, uelewa wa kina wa watu, kuchangia wazo na utambuzi kwa manufaa ya mteja.
RSM jijini Dar es Salaam imesherehekea siku hii kwa shughuli  mbali mbali za kijamii kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii. Timu imeianza siku kwa kuchangia damu katika Damu Salama. 

Wakati akihojiwa, Vile vile timu ya RSM, itajumuika na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mchanganyiko. “Watoto hawa wanahitaji mapenzi na misaada ya hali na mali. 

Sisi hapa RSM tunafurahia kuwaonyesha kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii yetu na wanathaminiwa katika ulimwengu huu.” Alisema Mtendaji Mkuu wa RSM.

 Shirika na wafanyakazi pia limeichangia shule vyakula mbalimbali na vifaa vingine kwa kwa ajili ya wanafunzi.


Kama sehemu ya kuendelea kusaidia sekta ya Elimu, RSM pia imechangia madawati katika jiji la Dar es Salaam kupitia  Kamati ya Madawati Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.
Chapa ya RSM inaiwezesha kuelezea vizuri uimara  na uwezo wake wa kutoa huduma duniani kote kama mshauri wa chaguo kwa soko la kati. Mtandao una mashirika katika zaidi ya nchi 120 na unajumuisha watu.



No comments

Powered by Blogger.