Watalaamu wa utafiti na wadau mbalimbali wa afya
kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo ya Naibu Waziri Wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamis Kigangwala hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa
watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini
Dar es salaam.
Na
Ally Daud-Maelezo
SERIKALI imesambaza chakula salama na kutoa tiba bure kwa
waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa sumukuvu katika mikoa ya Dodoma na Manyara
uliotokea hivi karibuni.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wakati
wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za
sumukuvu.
Dkt. Kigwangala alisema
Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapelekea vyakula salama waathirika wa ugonjwa
huo na kuteketeza vyakula vyenye sumukuvu.
"Tumepanga
utaratibu wa kupeleka vyakula salama kwa waathirika wa ugonjwa a sumukuvu
katika mikoa husika bila malipo ili kusaidia kuondoa ugonjwa huo na kuteketeza
mabaki ya vyakula vyenye vizaria vya sumukuvu" alisema Dkt. Kigangwala.
Aidha Dkt. Kigwangala
alisema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na waathirika wa sumukuvu ili
kuhakikisha wanaondoa ugonjwa huo kwani tayari umethibitishwa na wataalamu na
unapatikana kwenye mazao ya vyakula kama vile mahindi, uwele, mtama na karanga.
Kwa mujibu wa Dkt.
Kigangwala alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo Serikali imeamua kushirikiana
na wataalamu wa kimataifa ili kuweza kuondoa ugonjwa huo kwenye vyakula
vinavyolimwa nchini ili kuyawezesha mazao mazao hayo kuuzwa kwa urahisi hapa
nchini.
Dkt Kigwangala aliwashukuru
watafiti hao kwa kugundua chanzo cha ugonjwa huo ambao unasababishwa na Jamii
ya fangasi wanaoitwa Aspergillus wanaojikita zaidi kwenye vyakula na kuwataka
wapate matokeo chanya ya kutokomeza sumukuvu.
Naye Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Silo alisema katika mkutano huo watafiti
hao wanatarajia kujadili na kupata ufumbuzi wa tafiti za vyakula mbalimbali ili
visiendelee kuleta madhara kwa Watanzania.
|
Post a Comment