Watanzania 10 Kwenda Kufanya STARTIMES nchini China
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo.
Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmojawapo wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi wengine.
washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi.
Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha uwezo wake wa kuigiza sauti mbele ya majaji jukwaani.
Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza.
Mshiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza.
Na Dotto Mwaibale
Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.
Akizungumza baada ya shindano hilo Dar es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam ambaye ndiye aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji alisema kuwa anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho kwani haikuwa kazi rahisi.
‘’Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa watanzania kupitia kipaji change cha sauti.
Fursa niliyoipata mimi pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’ alisema Malecela
Fursa niliyoipata mimi pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’ alisema Malecela
‘’Napenda kuwaahidi watanzania kuwa nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya.
Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini.
Mara nyingi tumekuwa tukiona mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza lakini si kwa upande wa sauti. Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli ambayo inastahili kuigwa na makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo aliyeongoza kwa kuwa na alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji

Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na watanzania sehemu mbalimbali za nchi.
‘’Hatukutegemea kama watanzania wengi wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti.
Sanaa ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii mwenyewe anavyoamua anakitumia vipi kipaji alichonacho.
StarTimes tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili zinapendwa sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili tufanye nao kazi hiyo kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema Liao

‘’Tunaamini kupitia shindano hili tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10 watakaokwenda kujumuika na wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing, China katika kuzalisha kazi zilizo bora kabisa.
Nawasihi washindi waliopata fursa hii kuitumia vema kwa kufanya kazi kwa bidii kwani ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa na majaji kuwa vinara dhidi ya wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali.
StarTimes tunaahidi kuendelea na zoezi hili wakati ujao kwani bado uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote tupo kwa ajili ya kuwapatia kile wateja wetu wanachokitaka.’’ alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTime nchini

Katika fainali hizo washindi wa kwanza, pili na watatu; Hilda Malecela - kutoka DSM, Safiya Ahmed kutoka Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka Zanzibar) walizadiwa runinga za kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na 24 kila mmoja na StarTimes kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika fainali hizo huku washindi saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa kutoka StarTimes.
Kwa ujumla washindi kumi waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Sadiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao(DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM).
Na wote watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.
Na wote watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.
Katika mashindano hayo takribani washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika usaili uliofanyika katika mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar (Septemba 3) na Dar es Salaam (Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu wakabakia na kutinga hatua ya fainali.
Washiriki 18 waliotinga hatua ya fainali ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni Mathew Philip Mgeni, Dorcas Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na Hilda Kinabo; Zanzibar ni Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh, Rukia Hamdan, Imatu Obeid Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es Salaam ni Hilda Malecela, Abraham Richard, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel Landey, Coletha Raymond, Jamila Hassan na Maisala Abdul.
Post a Comment