Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini Joyceline
Lugora ( mstari wa mbele wa pili kushoto)
akikabidhi ufunguo wa jengo la ofisi ya Madini
Mkazi Wilani Tunduru mkoani Ruvuma, kwa Kamishna Msaidizi wa Madini
Kanda ya Ziwa Nyasa, Mhandisi Fred Mahobe,(
mstari wa mbele wa pili kulia) mara baada ya kukabidhiwa kutoka kiongozi wa timu ya ushauri ya ujenzi wa jengo
hilo, Msanifu Majengo Paul Mshana (kushoto katikati) aliyepewa dhamana ya
kusimamia ujenzi wa jengo hilo.
Na
Zuena Msuya, Tunduru ,RUVUMA,
Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Mradi wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) imepokea jengo la ofisi ya Madini
Mkazi wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Mkongo Contractors ili kuanza kutumika na ofisi hiyo baada ya
kufanyiwa ukarabati .
Akizungumza mara baada ya kupokea jengo hilo
wilayani Tunduru mkoani Ruvuma hivi karibuni, Msanifu Majengo wa SMMRP , Joseph
Ringo alisema kuwa lengo la kufanya ukarabati katika jengo hilo ni kuimarisha
shughuli za kiutendaji katika uendelezaji wa shughuli za madini wilayani ya Tunduru
na viunga vyake ukizingatia kuwa wilaya
hiyo imejikita zaidi katika uchimbaji wa madini ya vito vya aina mbalimbali.
Aidha Msanifu
majengo Ringo Alifafanua kuwa kama ilivyo dhamira ya mradi wa SMMRP ,kufanyika
kwa ukarabati katika jengo hilo kutawezesha Afisa Madini Mkazi wa eneo hilo
kufanya kazi zake kwa ufanisi na kufikia
malengo aliojiwekea katika kuwahudumia wadau wa madini.
Vilevile alisema kuwa ukarabati wa jengo hilo
umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia ambao umejumuisha vifaa vya kisasa ikiwemo kuunganishwa
na mfumo mpya na wa kisasa wa TEHAMA ambao unarahisisha utunzani wa kumbukumbu
za wadau wa madini tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Ofisa Madini mkazi Tunduru, Mhandisi
Fredrick Mwanjisi aliupongeza mradi wa SMMRP kwa kuboresha na kuzijengea uwezo
ofisi za madini nchini ili kuboresha shughuli za uendelezaji wa rasilimali za
madini.
Hata hivyo Mhandisi Mwanjisi ameushauri mradi wa
SMMRP,kutumia muda mfupi katika kutekeleza shughuli zake za ukarabati na ujenzi
wa majengo mbalimbali kwa lengo la kuendeleza rasilimali madini.
Naye Mkurugenzi Msaidizi rasilimali watu wa Wizara
ya Nishati na Madini,Joyceline Lugora, amewataka maafisa madini wakazi na
wakanda zote nchini kutunza miundombinu ya majengo hayo ili kuondoa gharama za
ukarabati wa mara kwa mara.
Na pia ichukue muda mfupi kukarabati eneo
lililoharibika endapo kumetokea uharibufu katika jengo.
|
Post a Comment