Wakuu Shule za Sekondari Waagizwa Kuwa na Kiwango cha Ufaulu Kuanzia Asilimia 41
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Shule za sekondari Wilayani humo.
Baadhi ya walimu wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi.
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa
shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu
kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na
kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye
weledi pasina mashaka.
Dc Ndejembi
amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo ikiwa
imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni kuonyesha
jinsi ambavyo walimu hawakujiandaa vyema katika kuwaimarisha wanafunzi
darasani ili kufikia ufaulu mahususi na kulijenga Taifa letu katika
misingi bora ya elimu.
Ndejembi alisema kuwa anataraji
kushirikiana na Afisa elimu sekondari ili kutoa hamasa kwa shule ambazo
zitafanya vyema katika mitihani yao ili kuamsha ari kwa shule zingine
Wilayani humo.
Walimu hao wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea,
kuwa na hofu ya Mungu, na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa katika
kufundisha wanafunzi kwani walimu wana wajibu mkubwa wa kuwafanya
wanafunzi kufaulu katika mitihani yao.
Sambamba na hayo pia Dc
Ndejembi amewataka walimu hao kutokuwa na madaraja kati yao na wanafunzi
wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi
kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo
yanayofundishwa na walimu hao.
Post a Comment