Viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila
kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze
mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro vikitokea Tunduma vikiwa kwenye gari lenye namba za usajili
T876 DDL aina ya DAF Leyland.
...................
Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na Maofisa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inamshikilia Dereva
Bw. Emanuel Bisama (37) ambaye ni mkazi wa Kimara Suka Dar es Salaam,kwa kosa la
kusafirisha magunia mawili ya mkaa ambayo baada ya kupekuliwa ndani yake kulikutwa na viroba viwili vyenye uzito kilo
50 kila kimoja vikiwa vimejaa bangi.
Akizungumza jana na
Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Pwani , ACP. Bonaventura Mushongi alisema Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland Bw. Emanuel Bisama (37) alikamatwa Septemba
21 saa 4.00 asubuhi katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoa
wa Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro akitokea Tunduma na kwa sasa yupo
mbaroni kwa mahojiano licha ya kukana
kuwa hakujua kilichomo ndani ya magunia hayo.
Kamanda Mushongi alisema
walifanikiwa kumkamata wakiwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa mazao ya Misitu
katika Barabara kuu ya Morogoro hadi Dare Salaam, aliongeza kuwa Dereva huyo wa
gari amefunguliwa kesi CHA/RB/3039/2016 kwa kosa la kupatikana na bangi.
Kwa upande Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania
(TFS) Kaimu wa Kanda ya Pwani Bw. Jonathan Mpangala alisema kuwa Mtuhumiwa huyo
amefunguliwa kesi ya pili yenye CHA/RB/5113/2016 kwa kosa la kumiliki na
kusafirisha mazao ya misitu bila kibali kwa sheria ya misitu namba 14 ya 2012
kifungu 88 na 89.
Alisisitiza kuwa Operesheni
ya kukamata usafirishaji wa mazao ya misitu bila vibali itakuwa ya kudumu baada
ya kuona magari mengi hasa makubwa yakiwa yamepakiwa magunia ya mkaa kuanzia
mawili hadi matano ambayo yamekuwa yakioneka waziwazi hata ukiwa barabarani namengi yakiwa hayalipiwa ushuru wa
Serikali kuu na hata magari mengine yakiwa hayajalipiwa ushuru wa Halmashauri.
( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii )
|
Post a Comment