Header Ads

Naibu Waziri ABDALLAH POSSI ahudhuria Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Wenye Ulemavu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha mada ya masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa wadau wa masuala hayo walipowasilisha Matokeo ya Tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano hoteli ya Serena Dar es Salaam Oktoba 12, 2016.
Mkalimani wa lugha ya alama Bw.Thomas Shayo akifasiri ujumbe kwa kundi la watu wenye ulemavu (wasiosikia) uliotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum uliofanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Mshiriki Rika (kundi la wazee) Bi.Elizabeth Nkwera akitoa mada ya usawa wa  huduma za kijamii kwa makundi maalum wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum ulioandaliwa na Mashirika ya misaada.

No comments

Powered by Blogger.