Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Ujumbe kutoka kampuni ya Dodsal Hydrocarborns inayofanya shughuli za
utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi
asilia nchini mara baada ya kumaliza kikao kilichojadili utekelezaji wa
shughuli za kampuni hiyo nchini. Kulia kwa Waziri ni Mmiliki na Mwenyekiti wa
kampuni hiyo, Dkt. Rajen
Kilachand na Watendaji wengine ni Shajee K.C (wa kwanza kulia), Salim Ajib (wa
pili kulia), na Dkt. Jogendra Sahu (wa kwanza kushoto).
Ujumbe
wa kampuni hiyo ambayo mwezi Julai, 2015 ilitangaza kugundua gesi ya kiasi cha
futi za ujazo trilioni 2.17 katika Bonde la mto Ruvu, ulikuja kuonana na
Profesa Muhongo ili kueleza mpango kazi wa shughuli zake hapa nchini.
Mwenyekiti
wa kampuni hiyo, Dkt. Kilachand aliwashukuru watendaji wa Wizara na TPDC kwa kushirikiana
na kampuni husika katika kuhakikisha shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi
na mafuta zinafanikiwa na kueleza kuwa kampuni hiyo inathamini ushirikiano ulipo
kati ya nchi za Tanzania na India na kuahidi kuuendeleza kwa kushirikiana
katika shughuli mbalimbali.
|
Post a Comment