Header Ads

Bodi Mpya ya NSSF yazinduliwa na Waziri JENISTA MHAGAMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameizindua rasmi Bodi ya Wadhamini wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Julai 5, 2016 Dar es Salaam.

Bodi hiyo imezinduliwa rasmi na kujadili mambo muhimu ikiwa ni kufikia malengo ya mfuko huo kwa kuzingatia masuala ya Utawala bora na ushirikiano ili kuchangia kukua kwa uchumi wa wananchi na kusaidia mahitaji ya wanachama wa mfuko huo.

Mhe.Mhagama aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa Bodi hii mpya ili kusaidia majukumu yote na kuhakikisha mafanikio yaliyopo yanakuwa ni chachu ya kuongeza kasi ya kufanya vizuri zaidi ili kuifikisha mahali pazuri zaidi.

“Ninawaahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali na kuamini kuwa Prof.Wangwe ameaminiwa na kupewa dhamana ya kutufikisha mahali fulani kwa kuisaidia bodi hii iliyozinduliwa rasmi leo.”Alisisitiza Mhe.Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Julai, 05, 2016.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 5, 16 Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Prof. Samwel Chacha Wangwe mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo Julai 5, 2016.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Samwel Chacha Wangwe alieleza kuwa, watajikita kwa kusaidia maeneo muhimu yenye changamoto kwa kuhakikisha wanaboresha na kuongeza wanachama wa Mfuko huo.

“eneo la Utawala bora utakuwa msingi wa kusaidia  mfuko uwe imara kwa kuzingatia kuwapa kipaumbele wanachama ili kuendana na kasi ya kukuza uchumi kwa kuzingatia kaulimbiu ya hapa kazi tu” Alisema Prof.Wangwe.

Mhe.Mhagama alimalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kufika na kushiriki katika uzinduzi huo, “nitoe shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote na kuwaomba tuwe kitu kimoja ili kuhakikisha shirika linatumia rasilimali zake ipasavyo ili kuwa na mapato ya kutosha.” Alisisitiza Mhe. Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) mara baada ya kuuzindua rasmi katika Ofisi yake Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.