Header Ads

Watendaji Watakiwa Kuhakikisha Usalama wa Rasilimali za Misitu

Na Mwandishi Maalumu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, amewataka watendaji katika ngazi za uteuzi nchini kushiriki kikamilifu katika kuhahikisha usalama wa rasilimali za misitu.

Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo leo katika Pori la Ruvu Kaskazini ikiwa ni siku ya Kitaifa ya kupanda miti na kueleza kuwa Serikali imekuwa na lengo la kupanda miti milioni moja nukta tano (milioni 1.5) kwa mwaka mzima katika kila wilaya, na kuwataka watendaji waliopo katika ngazi za uteuzi yaani Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu wakuu, kuhakikisha lengo hili linafikiwa na kueleza kuwa  viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili majina yao yatapelekwa katika mamlaka za uteuzi na kuchukuliwa hatua, hii ikiwa ni njia ya kupima usalama wa rasilimali hizi.

Akiongea na wananchi katika Pori la Ruvu Kaskazini, Mh. Mpina alisema kuwa asilimia 61 ya ardhi ya nchi ipo kwenye hatari ya kuwa jangwa kutokana na  uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti ovyo, na  takwimu zinaonyesha kuwa takribani hekta laki tatu nukta sabini na mbili za misitu zinakatwa kila mwaka kwa matumizi mbali mbali. “mikoa nane nchini iko hatarini kuwa jangwa”. Alisisitiza.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina  akipanda Miti katika Hifadhi ya Msitu  wa ruvu kaskazin uliyopo kibaha Mkoani Pwani mapema hii leo,wengine ni Baadhi ya wakurugenzi wakishuhudia Upandaji huo.

.................................

Akielezea athari, zitokanazo na  uharibifu wa misitu, Mh. Mpina alisema taifa linaweza kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununua chakula kuwalisha wa Tanzania kutokana na ukosekanaji wa mvua ,vyanzo vya maji kukauka, upatakinaji wa umeme kuwa wa kusuasua kutokana na uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji.

Kwa upande Mwingine Mh. Mpina alisema kuwa serikali imekata miti kwa sababu mbalimbali za msingi ikiwa ni pamoja ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, reli ujenzi wa bomba la gesi, hivyo basi kuna jukumu kubwa la kupanda miti mingi zaidi ya hiyo iliyokatwa.

Akitolea Mfano wa taasisi za huduma ya misitu Nchini (TFS) iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,  Mh. Mpina aliainisha kuwa taasisi zote za serikali zisaidie taifa kubainisha ni mazao  gani ya misitu yanaweza kupandwa katika maeneo gani kulingana na mahitaji ili kuweza kunusuru upotevu wa rasimali ya misitu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akitoa maelekezo kwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya  Maliasili na Utalii Injinia Angelina Madete( katikati) kuhusu upandaji miti katika sehemu mbalimbali katika hifadhi ya misitu kibaha Mkoani Pwani,mapema hii leo katika siku ya upandaji miti.

( Kwa Hisani ya EVELYN MKOKOI )

No comments

Powered by Blogger.