Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI akutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Mjumbe Maalum wa Rais wa GUINEA BISSAU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jenerali Umaro Sissico Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose’ Mario Vaz, Ikulu jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mjumbe huyo alileta salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Guinea Bisau.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua kutoka  Jenerali Umaro Sissoco Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau, Mheshimiwa Jose Mario Vaz. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau mara baada ya kupokea barua yenye Salamu na pongezi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jenerali Umaro Sissoco Embalo, Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau, Mheshimiwa Jose Mario Vaz, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
.........................................................................

Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose' Mario Vaz amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali, hususani katika uchumi kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.

Rais Jose' Mario Vaz amesema hayo katika ujumbe wa barua uliwasilishwa kwa Rais Magufuli na Mjumbe maalum wa Rais huyo Jenerali Omar Embalo, Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 25 Februari, 2016.

"Napenda kusisitiza kuwa nchi zetu ni marafiki wa muda mrefu, naomba urafiki na mahusiano haya mazuri yaendelee na ninakuhakikishia kuwa nchi yangu itaendelea kuuenzi ushirikiano huu" Ilieleza sehemu ya ujumbe huo.

Aidha, Rais Jose Mario Vaz amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano na amemualika kuitembelea nchi ya Guinea Bissau ili kuimarisha zaidi Uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Jose Mario Vaz kwa kumtuma mjumbe maalum kwa ajili ya kumletea ujumbe wa pongezi, na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Guinea Bissau.

"Nakushukuru sana Jenerali Umaro Sissoco Embalo kwa kuniletea ujumbe wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na nakuomba umwambie namshukuru kwa pongezi, mimi na serikali yangu tupo tayari kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Guinea Bissau ili mataifa yetu yaweze kunufaika zaidi"Alisema Rais Magufuli

Wakati huo huo, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Ikulu Jijini Dar es salaam leo.

Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Februari, 2016

No comments

Powered by Blogger.