Header Ads

Makamu wa Rais Mstaafu Dkt GHARIB BILAL akabidhi Zawadi kwa Washindi wa Mashindano ya QUR'AN Tukufu


Makamu wa Rais mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. 
 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

Picha na Mafoto Blog

No comments

Powered by Blogger.