Header Ads

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam SAID MECK SADIQ azindua Duka la HUAWEI





 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu. 
..................................

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea.



Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.



 Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 



"Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.



 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.



 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora jijini Dar es Salaam.



 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.



 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.



 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania, jijini Dar es Salaam. 
  
Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora. . Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.

Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.

Maisha ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao.

“Dar es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.

Alisema Mh Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa vifaa vya Huawei.

Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia  yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa  kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29 mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki, spika za Bluetooth na tisheti.

Huawei Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.

Maduka yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.

Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana.
Maduka ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa  teknolojia  katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa.


No comments

Powered by Blogger.