Header Ads

IGP ERNEST MANGU, AHUDHURIA IBADA YA KUSIMIKWA, ASKOFU WA KATOLIKI SINGIDA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akisalimiana na Mtawa wa kanisa katoliki pamoja na wananchi waliohudhuria  ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Mhashamu Edward Mapunda kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Singida jana,Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi Thobias Sedoyeka.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akisalimiana na watawa wa kanisa katoliki waliohudhuria  ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Mhashamu Edward Mapunda kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Singida jana.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone(kushoto) akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu (kulia) kabla ya kuanza ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Mhashamu Edward Mapunda kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Singida jana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimpongeza Askofu Edward Mapunda baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo katoliki Singida.Ibada hiyo ilifanyika jana mkoani Singida.

(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

No comments

Powered by Blogger.