Akinana Mama Wanaoshiriki Mradi wa Wanawake Katika Usukani ( WOW ) Wapewa Elimu
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifungua semina ya mafunzo ya haki za wanawake wanaoshiriki katika mradi huo iliyofanyika mwishoni mkwa wiki Kinondoni jijini Dar es salaam.
...............................................
Wanawake
wanaoshiriki katika mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) unaoendeshwa
na Kampuni ya AFREXA International Ltd, wametakiwa kufahamu haki
mbalimbali za binadamu zinamwongoza mwanadamu kushiriki vyema katika
shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza
Jijini DSM, wakati wa semina ya siku moja ya wanawake kuelekea katika
mafunzo ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara, mwanasheria kutoka
Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) WIGAYI KISSANDU amesema
ni muhimu kwa wanawake kufahamu haki hizo kwa kuwa zinatoa mwongozo
kufikia malengo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
MARTIN GABONE amesema semina hiyo ni moja ya hatua za mwanzo za mafunzo
ya udereva kwa wanawake kwa ajili ya kuendesha vyombo vya moto vya
biashara na kusisitiza wanawa wajibu wa kuhakikisha wanawake hao
wanaingia rasmi katika sekta ya usafirishaji kwa kuajiriwa au kujiajiri.
Mradi
wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) hadi sasa umesajili zaidi ya wanawake
200 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ili waweze kuwapatia bure mafunzo
ya udereva wa vyombo vya moto vya biashara ambapo baada ya mafunzo hayo
watatafutiwa ajira na wengine watawezeshwa ili waweze kujiajiri.
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akimtambulisha WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) mkufunzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akitoa mafunzo katika semina hiyo.
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mafunzo katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) na Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) wakiwa katika semina hiyo.
Post a Comment