AFCON 2017 : Uganda kumenyana na Ghana leo
Kocha wa Ghana Avram Grant amesema anataka kufika mbali zaidi katika
fainali za mwaka huu tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 walipofungwa na
Ivory Coast kwa njia ya penalti.
Mshambuliaji Asamoah Gyan na
kiungo wa West Ham Andre Ayew walikuwa miongoni mwao miaka miwili
iliyopita na uzoefu wao unatarajiwa kuwasaidia katika mchezo wa leo.
Wachezaji wa Uganda Murushid Juuko na Khalid Aucho wote hawatakuwepo katika mchezo huo.
Cranes wanaingia katika michuano hiyo tokea mwaka 1978 walipopoteza
dhidi ya Ghana katika hatua ya fainali, lakini wakati huu wanaingia
wakiwa ndio timu bora ya Afrika 2016.
Katika mchezo wa mwisho kwa
timu hizi kukutana zilitoka suluhu ya 0-0 na hapa ilikuwa kufuzu fainali
za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.
Ghana nao wanataka kushinda kombe hili ambalo hawajalipata tokea mwaka 1982.
Mafanikio makubwa kwa Uganda katika michuano hii ni ushindi wa pili miaka 39 iliyopita.
Ghana ni ya nane barani Afrika na ya 54 duniani wakati Uganda inashika nafasi ya 18 Afrika ya ya 73 duniani.
Post a Comment