Mwenyekiti wa Kikundi cha CHUHA Bi PILI ALLY akielezea Changamoto zinazowapata wakulima Wadogo wa zao la Miwa Wilayani Bagamoyo, baada ya Kuchelewa kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY utaowezesha Kujengwa kwa Kiwanda cha Sukari Katika Wilaya Hiyo.
Kuhusu tuhuma zinazotolewa na Wadau wa masuala ya
Mazingira kuhusu Kilimo cha Miwa kwenye Ukanda huo, wameiomba Serikali iliyo
chini ya Rais Dkt JOHN MAGUFULI kutuma wachunguzi ambao wamebobea kwenye suala
la Mazingira ili kujiridhisha na kutoa Baraka za kuanza kwa Mradi wa ECO
ENERGY.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiwangwa
akizungumzia juu ya tatizo hilo amesema vilio vya wakulima katika eneo lake ni vyema
vikatafutuwa ufumbuzi wa haraka.
Amesema kushughulikia mapema mgogoro huo kutawasaidia
Wakulima hao wadogo waliokopa fedha kwenye taasisi za Kibenki kurejesha mikopo
hiyo baada ya kuuza zao Miwa kwa mwekezaji wa Kiwanda kitakachojengwa baada ya
Kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY.
Wakati malalamiko
hayo ya wakulima yakitolewa uongozi wa mradi wa ECO ENERGY unaosimamia mradi huo,
Umesema tayari wameanza kupata hasara ya Kutupa Miwa ambayo imevunwa lakini
hakuna sehem ya kuipeleka kwa sababu ya kukosekana kwa Kiwanda kutokana na
kusuasua kwa mradi huo.
|
Post a Comment